Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Albert John Chalamila leo Oktoba 17, 2024 amecheza namba 9 katika mchuano mkali Kati ya timu ya Ofisi ya Mkoa na Shule ya Sekondari Kijitonyama ndani ya dakika 90 na kuibuka kidedea ambapo shule ya Sekondari ushiriki katika mechi maalum ya mpira wa miguu iliyofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Kijitonyama.
Bonanza Hilo maarufu kwa jina 'Chandimu Challenge' limefanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Kijitonyama Kisiwani lililolenga kuwa sehemu ya kampeni ya kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ambao unatarajiwa kufanyika hivi karibuni Tarehe 27/11/2024.
Vilevile kupitia mtanange huo uliohusisha mpira wa kikapu washindi kutoka Ofisi ya Mkoa walioiibuka kwa mabao 44 huku upande wa timu ya Shule ya Sekondari wakiambulia bao 5 tu. Mwisho wa michezo kupitia michuano hiyo washindi wa kwanza upande wa netball walipata kombe na pesa taslimu shilingi laki 500,000 huku washindi wa pili wakipata shilingi laki 250,000 na makombe sawa na washindi wa football.
Mwisho, bonanza hilo lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, walimu, wanafunzi,na wadau wengine
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa