Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Mei 13, 2024 amekabidhi Mwenge wa Uhuru 2024 Mkoa wa kusini Pemba-Zanzibar
Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Dar es Salaam ulipokelewa Mei 8, 2024 ukitokea Mkoa wa Pwani ambapo Mkoa wa Dar es Salaam umekimbiza Mwenge wa Uhuru katika umbali wa *KM 427.78 kwa kupitia miradi 39 yenye thamani ya Tsh 479,649,649,667 miradi ambayo baadhi ilikuwa imekamilika, na mingine katika hatua za utekelezaji
Aidha katika Wilaya zote tano za Mkoa huo Mbio za Mwenge wa Uhuru, zimetembelea, zimekagua, kuweka jiwe la msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo *miradi yote imepitishwa na Mwenge wa Uhuru 2024 hakuna mradi uliokataliwa
Vile vile Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Mkoa huo zimeelimisha na kuhamasisha wananchi kupitia Ujumbe wa " Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu"
Pia Ujumbe wa kudumu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kuhusu mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, Malaria, Dawa za Kulevya, Lishe na Rushwa
Sanjari na hilo Wilaya ya Ubungo ndio imehitimisha mzunguko wa Mwenge wa Uhuru katika Mkoa huo ambapo Mhe Albert Chalamila alikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Hassan Bomboko katika viwanja vya Barafu mburahati mapema leo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa