- Amesema Rais Dkt. Samia aliondoa zuio lililowakataza Bodaboda kuingia mjini kwa miaka mitano.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ametoa Ofa ya ufadhili wa ziara ya Mafunzo kwa Viongozi Machinga na Viongozi wa Shirikisho la bodaboda Mkoani humo kwenda Kigali Nchini Rwanda kujifunza na kujionea namna wenzao wanaendesha shughuli zao Za Biashara na usafishaji kwa kuzingatia Kanuni na taratibu.
Akizungumza wakati wa kikao Kazi kilichohusisha Viongozi wa Machinga, Bodaboda na Watendaji wa Serikali, RC Makalla amesema safari hiyo itahusisha Viongozi Watano wa Shirikisho la bodaboda na Viongozi watano wa upande Machinga ambapo kiongozi wa msafara atakuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Ludigija Ndatwa Ng'wilabuzu
Aidha RC Makalla amesema Tayari amefanya mawasiliano na Meya wa Jiji la Kigali Rwanda na Viongozi wa Machinga na Bodaboda wa nchi hiyo kwaajili ya kuwapokea na kuwatembeza maeneo mbalimbali ya Jiji Mwishoni mwa mwezi huu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa