-Awataka Wakurugenzi, Wakuu wa Wilaya na wadau wengine ndani na nje ya Mkoa kutumia bidhaa zinazozalishwa na kiwanda hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila amewataka viongozi Mkoani humo ikiwemo wakuu wa wilaya,wakurugenzi wa halmashauri na wakandarasi kutoka TARURA na TANROAD kutumia kiwanda cha taa cha SUMA JKT ili kupata taa bora zitakazowekwa katika jiji hilo na kuwezesha watu kufanya kazi usiku na mchana
RC Chalamila ameyasema hayo leo Novemba 12,2024 alipotembelea kiwanda cha taa kinachomilikiwa na SUMA JKT kilichopo Mlalakua Wilaya ya kinondoni ambapo pamoja na kuridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na jeshi hilo la kujenga Taifa ameagiza kiwanda hicho kitumike kama suluhisho la upatikanaji wa taa bora jijini humo.
Aidha RC Chalamila amewataka viongozi wa Mkoa huo kutumia kiwanda hicho kupata taa bora za kuweka maeneo mbalimbali ikiwemo barabarani na kwenye masoko kuwezesha biashara zifanyike usiku na mchana huku pia akitaka maabara ya kiwanda hicho kutumika kufanya majaribio ya taa zinazoingizwa kutoka nje ya nchi
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA JKT Brigedia Jenerali Petro Ngata amesema kiwanda hicho kinchojulikana jina la SUMA JKT SKYZON kinatengeneza taa za LED zinazotumia umeme na mfumo wa Solar na kwamba kwa ukanda wa Africa Mashariki hicho ni kiwanda cha kwanza kinachotengeneza taa bora na kinatarajia kuzinduliwa hivi karibuni hivyo amewataka wadau kutumia kiwanda high kupata taa
Mwisho RC Chalamila ametoa rai kwa watumishi wanaofanya kazi katika kiwanda hicho kufanya kazi kwa bidii pamoja na kuwa na uaminifu aidha kiwanda hicho kwa sasa kimesha anza uzalishaji na kinatarajiwa kufunguliwa raasmi hivi karibuni.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa