Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Oktoba 17,2023 amekutana na watoa huduma binafsi za Afya kwenye Mkutano wa pamoja uliofanyika katika Ukumbi wa Maktaba mpya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
RC Chalamila amewapongeza watoa huduma binafsi za Afya katika Mkoa kwa namna wanavyoshirikiana na Serikali kuwahudumia wananchi hususani katika Mkoa huo ambao ni lango kuu kwa ajili ya watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kufuatia Shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii.
Aidha RC Chalamila amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa sera nzuri ambazo leo zimetuwezesha kuwa hapa na uwekezaji mkubwa aliofanya na anaendelea kufanya katika sekta ya Afya, ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya Afya, Vifaa tiba, na hata kuwaendeleza kielimu wataalam hadi kufikia taaluma za kibingwa
Vilevile Mkuu wa Mkoa alipata wasaa wa kusikiliza kero na Changamoto mbalimbali ambazo zinaikabili sekta hiyo katika utekelezaji wa majukumu yake ambapo ameahidi kuzifanyia kazi zile zilizoko katika uwezo wake na zile kubwa atawasilisha katika mamlaka husika kwa Utekelezaji.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa APHFTA ( Association of Private Health Facilities in Tanzania) kanda ya Dar es Salaam Dkt Lazaro Wambura amemshukuru mkuu wa Mkoa kwa kuona umuhimu wa kukutana na kundi hilo wamefarijika sana na amewasilisha Changamoto zao kama watoa huduma binafsi za Afya katika Mkoa ikiwemo kutozwa tozo nyingi, na mfuko wa bima kulipa kwa kusuasua.
Mwisho RC Chalamila licha ya kufungua Mkutano huo amewataka washiriki wote kwenda kuelimisha jamii juu ya uwezekano wa kunyesha mvua kubwa za El-Nino kama ilivyotabiliwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), hivyo wananchi wachukue taadhari
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa