-Afanya kikao na watumishi wote wa Wilaya hiyo awataka kuchapa kazi kwa weledi.
-Akagua miradi ya elimu, Afya, Barabara na Kuongea na Wananchi katika viwanja vya Maturubai-Kizuiani
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa leo Octoba 05,2024 ameanza ziara katika Mkoa wa Dar es Salaam Wilaya ya Temeke kukagua miradi ya maendeleo na kisha kuongea na wananchi kupitia Mkutano wa Hadhara alioufanya katika viwanja vya Maturubahi Mbagala wilaya ya Temeke.
Mhe Kassim Majaliwa akiongea na watumishi wa Wilaya hiyo amewataka kuwahudumia vizuri wananchi, kupunguza urasmu, kujipanga kuondoa umasikini kwa wananchi kwa kuhakikisha wanapata huduma muhimu kama vile maji na umeme pia kuratibu vizuri makundi maalum ikiwemo wazee.
Aidha Waziri Mkuu amesema Serikali ya Dkt Samia inaendelelea kuboresha stahiki za watumishi ambapo amewataka kufanya kazi kwa weledi mkubwa.
Sambamba na hilo Waziri Mkuu amefungua Hostel ya kisasa katika shule ya Sekondari Kibasila ambapo amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii kwa kuwa Mhe Rais Dkt Samia ameshaboresha kwa kiasi kikubwa mazingira ya kufundishia na kujifunzia.
Sanjari na hilo Mhe Kassim Majaliwa amekagua mradi wa barabara inayoelekea bandari ya DSM , Ujenzi wa Hospitali ya Ghorofa 6 Mbagala na kisha kuongea na wananchi ambapo amewataka wananchi kuendelea kumuunga Mkono Rais Dkt Samia kwa kuwa jitihada zake za kuwaletea maendeleo wananchi zinaonekana.
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila akitoa salamu za mkoa amesema Mkoa uko shwari na amemshukuru Rais Dkt Samia Sukuhu Hassan kwa kuendelea kutoa pesa nyingi ambazo zinatekeleza miradi mbalimbali katika Mkoa huo kwa maslahi mapana ya ustawi wa jamii.
Mwisho Mhe Kassim Majaliwa anatarajiwa kuendelea na ziara yake Octoba 06, 2024 Katika Wilaya ya Kigamboni.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa