Mhe Dkt Dorothy Gwanyima Akiwa katika picha ya pamoja na watoto wa shule ya msingi baada ya uzinduzi huo Karimjee DSM
- Asema Uzinduzi wa Mabaraza na Madawati ya Ulinzi na Usalama wa Watoto DSM ni kwa niaba ya Mikoa mingine yote ya Tanzania Bara
-Apongeza Mkoa wa DSM kwa kufikia 90% ya uundaji wa Mabaraza na Madawati ya Ulinzi na Usalama wa Watoto
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Mhe Dkt Dorothy Gwajima leo amezindua Mabaraza na Madawati ya Ulinzi na Usalama wa Watoto katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam.
Waziri Gwajima amesema Uzinduzi huo katika Mkoa wa Dar es Salaam ni kwa niaba ya Mikoa mingine yote ya Tanzania Bara.
Hata hivyo Waziri Gwajima amesema Mabaraza na Madawati ya Ulinzi na Usalama wa Watoto yameundwa kwa lengo la Kuimarisha Utekelezaji wa Haki, Ulinzi na Ustawi wa mtoto nchini Serikali kupitia Wizara yenye dhamana na watoto iliandaa sera ya maendeleo ya mtoto ya mwaka 2008 ambayo imeainisha haki 5 za msingi za mtoto
Haki hizo ambazo ni *Kuishi, Kulindwa, Kuendelezwa, Kushiriki na Kutobaguliwa vilevile wizara imeratibu utungwaji wa sheria ya mtoto Na 21 ya mwaka 2009 na sasa inafanya mapitio ya baadhi ya vipengele vya sheria hiyo na kanuni zake ili iweze kukidhi mahitaji kwa ajili ya ustawi wa watoto.
Aidha Mhe Dkt Dorothy Gwajima ameupongeza Mkoa wa Dar es Salaam kwa kufikia 90% ya uundaji wa mabaraza na madawati ya Ulinzi na Usalama wa Watoto ambapo *jumla ya Mabaraza ya Watoto 377 na Madawati ya Ulinzi na Usalama ni 776 hivyo Mabaraza na Madawati yaliyoanziswa ni 1,153 sawa na asilimia 90 ya madawati yote yanayopaswa kuundwa katika Mkoa wa DSM.
Baadhi ya wasanii ambao ni mabalozi wa kupinga ukatili dhidi ya watoto nchini wakiwa katika ukumbi wa Karimjee-DSM
Waziri Mhe Dkt Dorothy Gwajima ameitaka jamii kushirikiana na Serikali kupambana na ukatili dhidi ya Watoto hapa nchini, kwa kutoa elimu au taarifa pale wanapoona vitendo vya ukatili vinafanyika.
Hafla hiyo ya *Uzinduzi wa Mabaraza na Madawati ya Ulinzi na Usalama wa Watoto imeudhuriwa na watoto wa Shule za msingi, Wasanii ambao ni mabalozi wa Kataa ukatili dhidi ya Watoto, wataalam kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Maafisa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii wa Halmashauri za Mkoa huo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa