-Wampa Tuzo ishara ya shukrani
-RC Makalla amemshukuru Rais Samia Kufanikisha SENSA
-Mkoa wapanga kujenga "Dropping Centre" ya watoto wa mitaani na ombaomba kuwawezesha kusoma na kujiajiri
Watoto hao wa Mitaani au wanaoishi katika Mazingira Magumu wametoa shukrani hizo leo Octoba 12,2022 katika Ukumbi wa Diomond Jubilee wakati wa *Warsha ya watoto wanaoishi katika Mazingira Magumu na Tathimini ya Sensa ya Mkoa wa Dar es Salaam
Aidha wamekabidhi Tuzo maalum ishara ya shukrani kwa kutambuliwa, kuthaminiwa, kupatiwa fursa ya kuhesabiwa wakati wa zoezi la SENSA 2022 na kujumuishwa katika Takwimu ya Taifa lao fursa ambayo hawakuwai kuipata Kipindi cha nyuma.
Sambamba na hilo RC Makalla wakati wa warsha hiyo amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha Zoezi la Sensa ya watu na Makazi kufanyika kwa Utulivu na kisasa zaidi kuliko wakati wowote ambapo Makundi Maalum ambao ni watoto wanaoishi katika Mazingira Magumu wakijumuishwa katika Takwimu ya Taifa.
Pia RC Makalla amesema zoezi la SENSA DSM limefanyika vizuri, amempongeza Kamisaa wa Sensa Tanzania Bara Mhe Anna Makinda , Mratibu wa Sensa katika Mkoa huo na Wananchi kwa Ujumla kwa kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo.
Hata hivyo RC Makalla amepokea Tuzo Maalum ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu kutoka kwa vijana wanaotoka katika Mazingira magumu ikiwa ni shukrani yao kwa Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ameahidi kuwasilisha Tuzo hiyo.
RC Makalla amesema Mkoa una mpango wa kujenga "Dropping Centre" ya watoto wa mitaani na ombaomba ili kuwawezesha kusoma na kujiajiri kwa mfano kama mtoto ana kipaji cha mpira, ufundi, sanaa, hata kusoma ndani ya Kituo hicho atatambuliwa na kuwezeshwa kutokana na kipaji chake tayari RC Makalla ameshamuelekeza Mkurugenzi wa Kigamboni kutenga eneo kwa ajili hiyo
RC Makalla amewataka maafisa Ustawi DSM kufanya Kazi kwa karibu na NGO'S zinazosaidia makundi maalum kama vile James Foundation na kusema tayari ameshamuelekeza Katibu Tawala Mkoa kupitia Risala iliyosomwa na kuanisha mambo yote muhimu kwa ajili ya Utekelezaji mapema iwezekanavyo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa