Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amewataka wananchi wa Mkoa huo kuchukua tahadhari ya El-Nino inayotarajiwa Kipindi cha mvua za vuli Oktoba-Novemba 2023 kama ilivyo tabiliwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)
Mvua hizo zinatarajiwa kuanza wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Oktoba 2023 na kuisha wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Januari 2024
Aidha RC Chalamila amezitaka Halmashauri zote, Taasisi, Wadau, wananchi kwa Ujumla kuchukua tahadhari dhidi ya hali hiyo ya El Nino.
Mwisho Mkoa unawasisitiza wananchi kufuatilia utabili wa Hali ya Hewa unaotolewa na Mamlaka husika saa 24 siku 5, Siku 10 na Siku 30 na kuzingatia ushauri unaotolewa vilevile wanakumbushwa kutodharau nguvu ya maji kwa kutovuka Wala kuingia katika madimbwi amabayo kina chake hakifahamiki au kuogelea katika mito, bahari, katika Kipindi chote cha El-Nino
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa