- Awataka kufanya kwa dhati majukumu yao ya Usafi
- Kuwa na wafanyakazi wenye uwezo na vitendea kazi vizuri
- Kila mkandarasi awe na Mawasiliano na Mkurugenzi, kwa maana ya namba ya simu ili aweze kutoa taarifa ya hali ya Usafi mfano uwepo wa wafanyabiashara holela katika eneo lake
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo Disemba Mosi, 2021 amefanya kikao kazi na Wadau muhimu wa Usafi na Uhifadhi wa Mazingira katika Ukumbi wa Anatoglo Ilala-Dar es Salaam.
Kikao kazi hicho kimelenga kutoa maelekezo kwa wadau hao ambao ni *wakandarasi wa Usafi kutoka katika Manispaa zote za Mkoa wa DSM ili kufanikisha Kampeni kabambe yenye kauli mbiu SAFISHA PENDEZESHA DAR ES SALAAM
Miongoni mwa mambo mengi aliyoelekeza *RC Makalla* amewahakikishia wakandarasi hao kuwa anazifahamu Changamoto zao ikiwemo kuwepo kwa mikataba ya mda mfupi, ulegevu wa ulipaji ada za taka, na kutolipwa kwa wakati na nyingine nyingi lakini kupitia dhamira yake Kuliweka Jiji Safi tayari ameshotoa maelekezo kwa ajili ya Utekelezaji.
RC Makalla amewataka wakandarasi kufanya usafi kweli kweli pasiwepo na Uchafu katika eneo ambalo mkandarasi amekabidhiwa
Mkuu wa Mkoa amesisitiza wakandarasi hao kuwa na wafanyakazi wenye sifa na uwezo wasiwe wazee ambao hawana uwezo wa kufanya kazi pia Kampuni za Usafi ziwe na vifaa vizuri pasiwepo na Magari mabovu au ambayo na yenyewe ni taka.
Aidha RC Makalla amewataka wakandarasi wote kuwa na namba za simu za Wakurugenzi husika ili kuweza kutoa taarifa pale wanapokuta kuna wafanyabiashara holela, watu wanaotiririsha maji na uchafuzi mwingine wowote wa Mazingira ili uweze kudhibitiwa.
" SAFISHA PENDEZESHA DAR ES SALAAM " USAFI UNAANZA NA WEWE.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa