Zaidi ya Kampuni 70 za ukandarasi zimejitolea kujenga mitaro ya barabara mbalimbali za Dar es salaam Bure kama sehemu ya kuunga mkono jitiada za Mkuu wa mkoa huo Mhe. Paul Makonda.
Hatua hiyo imekuja baada ya RC Makonda kufanya ziara usiku na mchana na kujionea uharibifu mkubwa wa barabara uliotokana na ukosefu wa mitaro ya maji na kuamua kuwashirikisha wakandarasi ambao walipokea kwa mikono miwili ombi hilo.
RC Makonda amewaagiza wenyeviti wa mitaa kuratibu idadi barabara zisizokuwa na mitaro kwenye mitaa yao kisha kupeleka kwa Meneja wa TARURA Wilaya kwa ajili ya kupatiwa kampuni itakayojenga mitaro hiyo.
Aidha RC Makonda amezishukuru kampuni zilizojitolea kujenga mitaro hiyo Bure jambo litakalosaidia kuokoa mabilion ya pesa za serikali.
Kwa upande wao wakandarasi wamesema wamejiandaa vizuri kuanzia vifaa na wataalamu kwa ajili ya ujenzi huo huku baadhi yao wakiwa tayari wameanza ujenzi kwenye baadhi ya mitaa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa