Katika kuunga Mkono juhudi zinazofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda katika kusaidia Watu wenye uhitaji wa miguu bandia na zoezi la upimaji wa Afya, Kampuni ya China National Building Material Group leo imekabidhi Hundi ya Shilingi Milioni kumi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kupokea msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mganga Mkuu wa Mkoa Dakta Grace Magembe amesema Serikali ya Mkoa imekusudia kutatua changamoto za kiafya kwa wananchi pamoja na kusaida watu wenye ulemavu, ambapo amebainisha kuwa hapo awali Serikali ya Mkoa ilikusudia kusaidia watu wenye ulemavu wapatao miambili lakini idadi ya wenye uhitaji wa miguu ni zaidi ya watu elfu moja hivyo amewataka wadau kuendelea kujitokeza kusaidia.
Dakta Grace Magembe ameongeza kuwa tokea kuingia madarakani Serikali ya awamu ya tano ilio chini ya Rais Dakta John Pombe Magufuli imekuwa ikishughulikia changamoto mbalimbali za wananchi hivyo amewataka wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi hizo.
Kwa upande wake Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya China National building Material Group Wang Shupeng amesema kampuni hiyo imeridhishwa na juhudi zinazofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na imetambua umuhimu wa kusaidia watu wenye mahitaji maalumu ikiwemo miguu bandia hivyo mbali na msaada huo wa shilingi milioni kumi za kitanzania itaendelea kutoa misaada mbalimbali kwa Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa