- Wampongeza kwa Uamuzi ya kuwapeleka Viongozi wa Machinga na Bodaboda Nchini Rwanda kujifunza.
- Wasema anayaishi vizuri maono ya Rais Dkt. Samia.
- Awataka SHIUMA Taifa na Viongozi wa Machinga DSM kushirikiana
Viongozi wa Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania SHIUMA wamefunga safari mpaka Mkoa wa Dar es salaam kumpongeza Mkuu wa Mkoa huo CPA. Amos Makalla kwa ushirikiano Mkubwa anaowapatia Machinga ikiwemo kuwasafirisha Viongozi wa Machinga na Bodaboda Nchini Rwanda kujifunza na uongozi rafiki kwa kundi la Machinga.
Miongoni mwa Viongozi hao ni pamoja na Mwenyekiti wa SHIUMA Taifa Ndg.Matondo Masanja, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na Viongozi wa SHIUMA Mkoa wa Dar es salaam.
Akizungumza wakati wa kikao na Viongozi hao, RC Makalla amepokea maombi ya Viongozi wa SHIUMA Taifa ikiwemo Viongozi wa Taifa kupata fursa ya kusafirishwa Nchini Rwanda kujifunza, ombi la Kikao na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na ombi kufanyika Mkutano Mkuu wa Machinga Tanzania kufanyikia Dar es salaam.
Aidha RC Makalla Ameahidi kufanyia kazi ombi la Viongozi hao kukutana na Rais Dkt. Samia ambapo amesema atawasiliana na Mamlaka husika ili kufanikisha jambo Hilo.
Pamoja na hayo RC Makalla ametoa wito kwa Viongozi wa SHIUMA Taifa kufanya kazi kwa pamoja na Viongozi wa SHIUMA Mkoa wa Dar es salaam Ili kwa pamoja waweze kuinua na kushughulikia changamoto za Machinga.
Hata hivyo RC Makalla ameendelea kutoa wito kwa Machinga kuendelea kufanya biashara kwenye Maeneo Rasmi Ili waweze kunufaika na fursa za mikopo ambapo amesema Serikali Itaendelea kushughulikia changamoto zozote zitakazojitokeza.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa