Mhe Amos Makalla akisoma bango mara baada kuzindua mfumo huo katika ukumbi wa mikutano DMDP Ilala Jijini Dar es Salaam.
-Asema mfumo huo wa kidigitali utaongeza makusanyo na kudhibiti upotevu wa mapato ya maegesho
-Mfumo huo pia utapunguza kero kwa wananchi
-Awaonya vishoka wa maegesho kuacha mara moja kwa kuwa mfumo huo ndio mwarobaini kwao
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa ukusanyaji wa ushuru wa maegesho kwa njia ya mtandao(kidigitali) mapema leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla amezindua mfumo wa kidigitali kukusanya ushuru wa maegesho kwa Mkoa wa Dar es Salaam unaojulikana kwa jina la "termis" unaotarajiwa kuanza rasmi septemba mosi 2021
Hafla ya uzinduzi huo imefanyika leo Agosti 24, 2021 katika ukumbi wa mikutano wa DMDP Ilala Jijini Dar es Salaam.
Akifungua hafla ya uzinduzi wa mfumo huo Mhe Amos Makalla amewapongeza TARURA kwa kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2021 ya matumizi sahihi ya TEHAMA ili kuchochea maendeleo.
Mhe Makalla amesema kutokana na mfumo huo wa kidigitali wa kukusanya ushuru wa maegesho utadhibiti upotevu wa mapato hivyo matarajio ni kuwa na makusanyo makubwa au mapato kuongezeka zaidi na zaidi.
Vilevile mfumo huo utaondoa kero kwa wananchi kwa kuwa sasa wanaweza kufanya malipo kiganjani kwa kutumia simu janja yaani "Smartphone".
Aidha Mhe Mkuu wa Mkoa amewaelekeza TARURA kuweka mabango katika maeneo ya maegesho ili kuepusha usumbufu usio wa lazima kwa wananchi wa "wrong Parking"
Sambamba na hilo Mhe Makalla ameendelea kutoa onyo kwa vishoka wanaokusanya ushuru wa maegesho katika Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwa mfumo umepatikana ametoa rai wananchi kuutumia mfumo wa kidigitali ndio utakomesha biashara ya vishoka hao wa maegesho.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa