Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameyasema hayo leo Septemba 16, 2023 wakati wa maadhimisho ya siku ya usafi Duniani katika viwanja vya Zakhiem Mbagala Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam.
RC Chalamila amekemea tabia za kuto zingatia taratibu za usafi kama vile mtu amepanda kwenye gari la Umma akula kitu baadae anatupa barabarani bila aibu pia kufanya biashara maeneo yasiyo rasmi na hata madereva wa bodaboda wanavyopaki ovyo barabarani amesema kituo chochote kikiwa mahali pasipo sahihi ni Uchafu hivyo usafi ni pamoja na mtu kuwa katika eneo lake stahiki.
Aidha Mhe Chalamila amesema suala la usafi lazima liwe ajenda ya kudumu katika Wilaya zote za Mkoa huu, pawepo na mjadala mpana katika vikao mbalimbali vya Halmashauri vilevile Usalama wa Mkoa ni ajenda za kudumu katika Mkoa zingine zinafuata " Taka ni Uchafu na Uchafu ni maradhi, tengenezeni By Laws za kudhibiti uchafu na jamii lazima itii sheria bila shuruti " Alisema RC Chalamila
Vilevile Mhe Mkuu wa Mkoa amesema Mhe *Selemani Jafo* alitakiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo kutokana na sababu zisizo zuilika ameshindwa kuja hivyo ameniagiza niwaambie yuko pamoja nanyi na anawashukuru kwa namna mnavyounga mkono utekelezaji wa majukumu yake katika wizara anayoiongoza, ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Rais Muungano na Mazingira.
Sambamba na hilo maadhimisho hayo yameongozwa na kauli mbiu "Tuungane Pamoja Kujifunza Kupanga na kuhimiza Uimarishaji Huduma za Udhibiti wa Taka" ambapo *Mhe Chalamila* ameshiriki kufanya usafi na kujionea maonyesho mbalimbali na namna ya kuthibiti taka ambayo yalikuwa yanaonyeshwa na wadau wa Mazingira katika viwanja hivyo na baadae kukabidhi tuzo kwa makundi mbalimbali ishara ya kutambua mchango wao katika usimamizi wa mazingira
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe Mobhare Matinyi amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kuendelea kusimamia usafi katika wilaya Temeke kwa kufanya hivyo ni njia nzuri ya kuzuia magonjwa milipuko na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Ifahamike kuwa maadhimisho ya siku ya usafi Duniani huadhimishwa kila jumamosi ya wiki ya tatu Septemba kila mwaka na kwa Tanzania mara ya kwanza maadhimisho hayo yalianza kuadhimishwa mwaka 2008
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa