Mkuu wa Mkoa wa Da es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda amekutana na Balozi Wa Korea kusini Nchini Tanzania na kufanyanae mazungumuzo juu ya maombi ya Ofisini kwake kwa shirika la KOICA katika kujenga Hospitali ya kisasa ya mama na mtoto kama waliomjengea Chanika yenye thamani ya Bilioni 8.8 katika wilaya mbili mpya yani wilaya ya Ubungo na wilaya ya kigamboni ili kusaidia wakina mama na watoto.
Maombi hayo yamepokelewa ikiwa ni mwendelezo wamajadiliano yaliyofanyika kati ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam na wabunge Wa Korea Kusini mwaka Jana walipokuja kutembelea mradi Wa Hospitali ya mama na mtoto yenye uwezo wa kulaza watu 161, vitanda vya kuhifadhi watoto njiti 60, uwezo wa kufanya oparesheni 4 kwa wakati mmoja na pia sehemu za mapumziko ya wamama wanaojiandaa kujifungua 100, huku ikiwa na nyumba za watumishi wa familia 28 katika eneo hilo hilo la kazi kama sehemu ya kuongeza tija katika utoaji Wa huduma.
Ujenzi wa Hospitali hizi nyingine mbili kwa wilaya lengwa ukifanikiwa utagharimu takribani shilingi Bilioni 17.6 za kitanzania mpaka kukamilika. “Naendelea kumwamini Mungu kwa kazi aliyonipa”, alisema Mkuu wa Mkoa.
Wilaya ya Ubungo na Wilaya ya Kigamboni Neema inakuja kwa kina mama na watoto.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa