Mhe Makalla akiongoza kikao kazi na Viongozi wamachinga mapema leo Jijini Dar es Salaam.
- Wamsifu kwa kupokea maagizo ya Rais na kufanya kikao shirikishi na Uongozi wa Machinga
- Wamekiri kuwepo kwa biashara holela Dar, na kuahidi ushirikiano na Serikali
- Mhe Makalla awahakikishia Machinga hakuna atakayekosa sehemu "nimejipanga vizuri"
- Asema kesho septemba 17,2021 atazindua rasmi mpango wa kuwapanga wamachinga DSM
Uongozi wa Wamachinga Mkoa wa Dar es Salaam umefurahishwa na Kikao cha RC Makalla na Viongozi wa Machinga* kuhusu kuwapanga Machinga katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mkutano wa Mkoa na kuhudhuriwa na Waheshimiwa wakuu wa Wilaya, Kamati ya ulinzi na Usalama, Sekretarieti ya Mkoa na Viongozi wa Wamachinga kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam.
Akiongea wakati wa kikao hicho Makamu mwenyekiti wa wamachinga Taifa Ndg Steven Silinde kwa niaba ya wenzake amesema amefurahishwa na namna RC Makalla alivyojipanga kuwapanga wamachinga DSM
" Kikao kazi cha leo kimekuwa shirikishi nasi viongozi wa Wamachinga tumetoa maoni yetu kwa uwazi tukiwa huru, tunamhakikishia Mkuu wa Mkoa Ushirikiano uliotukuka" Alisema Ndg Lusinde
Akaendelea kufafanua siku za nyuma maagizo ya Kitolewa na Rais yamekuwa yakitekelezwa bila kutushirikisha viongozi wa Wamachinga lakini Mkuu wa Mkoa ametuita na kuongea nasi kwa namna hiyo tunampongeza RC Makalla na tunamuahidi ushirikiano mzuri katika jambo hilo alisisitiza Ndg Lusinde
Aidha Mhe Makalla akiongea wakati wa kikao hicho amebainisha yeye binafsi alishafanya utafiti wa kutosha juu ya biashara holela DSM, amewataka viongozi hao kumpa ushirikiano.
Akasisitiza Machinga ni taasisi muhimu hakuna mmachinga atakosa sehemu ya biashara, watapangwa vizuri na kesho septemba 17,2021 nazindua rasmi mpango wa kuwapanga wamachinga DSM ndani ya mwezi mmoja kama waziri Mkuu alivyoelekeza wamachinga watakuwa wamepangwa Alisema Mhe Makalla
# Dar es Salaam isiyo na wafanyabiashara holela inawezekana kikubwa ni ushirikiano kwa maslahi mapana ya Mkoa na Taifa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa