Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa Pamoja na Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila leo Novemba 13, 2023 wamefika katika barabara ya Kikwete High way itokayo Kimara mwisho kuelekea Bonyokwa kuona changamoto zinazowakabili watumiaji hususani katika Kipindi hiki cha mvua ambacho kimechangia uharibifu mkubwa
Wananchi walijitokeza kwa wingi kuelezea kero na changamoto wanazopata zikiwemo kukosa huduma ya afya, nauli za bajaji na bodaboda kupanda, biashara zao kukwama na zaidi kila mwaka wanapewa majibu ya kiasa wanapohitaji utatuzi wa changamoto zao.
Mhe Innocent Bashungwa aliwahakikishia wananchi wa maeneo hayo kwamba mkandarasi anatakiwa kuanza ujenzi wa barabara hiyo yenye KM 7 kwa kiwango cha lami mwezi Desemba mwaka huu pia ametoa agizo ujenzi wa dharura uanze mara moja, "Ninakuelekeza meneja TANROAD gusa mfuko wako wa dharura tafuta mkandarasi ambaye wakati wananchi wamelala yeye anatengeneza hii barabara."
Mhe. Chalamila alitilia mkazo suala la ujenzi huo uanze muda huohuo kwa kuagiza meneja wa TANROADS abaki pale kuanza kazi na ifikapo kesho jioni atapita kukagua na kuwachukulia hatua iwapo hawatafuata maelekezo waliyopewa, "Kwakuwa Mhe Waziri amesema wakatafute hela ya dharura, nataka niwaahidi kesho jioni, saa mbili ya usiku nitakuwa hapa," alisema RC Chalamila.
Vilevile RC Chalamila amewataka watumie 'molam' ili kuepuka utelezi kwa watumiaji, ni muhimu kurudisha mawasiliano kati ya pande hizo mbili, matatizo wanayokumbana nayo ni makubwa na Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan bado ana mipango mingi ya utoaji wa fedha ili kuendelea kutatua kero za muda mrefu na zile za muda mfupi kwa mwananchi.
Naye mbunge wa jimbo hilo la Ubungo Prof. Kitila Mkumbo alisema kwamba wananchi wanapokuwa na shida wana haki yakuwalaumu viongozi wao na kuwaomba wawe na subira kwakuwa barabara hiyo imeshaingia kwenye mpango na suala hilo lishafika bungeni na ipo kwenye bajeti.
Awali mhe. Bashungwa na RC Chalamila walifanya ziara kata ya Kibamba na kukagua ujenzi wa barabara inayoanzia Kibamba Shule kuelekea Mpiji Magohe yenye urefu wa KM 9.2 ambayo ishakamilika KM 2 huku KM 1.5 ujenzi wake unaendelea. Sambamba na hapo walifika mpaka Kiluvya kukagua mchakato wa ujuenzi wa barabara ya mwendo kasi inayotarajiwa kufika mpaka kibaha
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa