# Ahimiza kuzingatia mwongozo uliotolewa na Wizara ya afya katika kukabiliana na ugonjwa wa UVIKO-19
# Kusitisha mikusanyiko isiyo ya lazima
# Vyombo vya usafiri kuzingatia "Level seat"
# Kuwepo kwa maji tiririka na vitakasa mikono katika maeneo mbalimbali ya mikusanyiko
# Uvaaji barakoa ni lazima
Mhe Amos Makalla ameyasema hayo baada ya kufanya kikao na kamati ya ulinzi na Usalama cha tathimini ya utekelezaji wa mwongozo wa Wizara ya Afya katika kukabiliana na UVIKO-19 kwa Mkoa wa Dar es Salaam toka alipotoa tamko mara ya kwanza.
Mkuu wa Mkoa amebainisha kuwa kwa Mkoa wa Dar es Salaam yako maeneo tahadhari inachukuliwa vizuri lakini maeneo mengine bado
"Mfano mtu avaa barakoa anapoingia kwenye kivuko au daladala akiwa ndani anavua hiyo sio sahihi ukijikinga wewe unamkinga na mwenzako" Alisema Mhe Makalla
Aidha ifahamike kuwa Mkoa wa Dar es Salaam una idadi kubwa ya watu na muingiliano mkubwa wa watu kila mmoja akichukua taadhari ni rahisi kupunguza kasi ya kuenea kwa ugonjwa huo.
Vilevile Mhe Mkuu wa Mkoa amewataka wakuu wa Wilaya katika maeneo ya kupitia kamati zao za ulinzi na usalama kusimamia utekelezaji wa mwongozo wa kukabiliana na UVIKO-19.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa