Akizindua huduma hiyo ya kibenki kwa watu wasio ona leo Novemba 17, 2023 katika Tawi la Benki hiyo Kijitonyama Wilaya ya Kinondoni, Mkuu Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameipongeza Benki hiyo kwa ubunifu ambao unafungua fursa za kibenki kwa kundi maalum la watu wasiona na imekuwa Benki ya kwanza hapa nchini kulifikia kundi hilo muhimu.
Aidha ameitaka menejimenti ya Benki hiyo kuendelea kuwa na ubunifu, kutanua wigo wa soko la Benki kwa kuongeza matawi, kuwa na wahudumu wazuri watakao hudumia watu wenye ulemavu, kuwa na mkalimani na kuendelea kutoa huduma rafiki katika kundi hilo maalum "UBA Benki mmewatendea haki watu wasiona, Benki hii ni nzurii watumishi kuweni waadilifu endeleeni kufanya Kazi kwa bidii" Alisema RC Chalamila
Aidha Mtendaji Mkuu wa Benki ya UBA Bwana Gbenga Makinde amesema kwa sasa UBA ina matawi mnne, dhamira ya Benki ni kutoa huduma bora za Kibenki kwa Watanzania hususani wakazi wa Dar es Salaam kwa kuzingatia mahitaji ya makundi yote.
Ifahamike kuwa Serikali ya Awamu sita chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan imekua ikitoa kipaumbele kwa makundi maalum hapa nchini kwa kuboresha huduma zao katika nyanja mbalimbali ikiwemo uwezeshaji makundi hayo kiuchumi hivyo UBA Benki imeenda sambamba na dhamira ya Mhe Rais ambapo kupitia huduma hiyo sasa watu wenye ulemavu wa kutoona wamepatiwa fursa adhimu ya kufanya miamala ya kibenki
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa