- Asema Mhe Rais Samia Suluhu anaheshimu sana viongozi wa Dini na anathamini mchango wao
- Asisitiza Umuhimu wa kuombea Nchi Amani, Upendo na Umoja pasipo kusahau Kumuombea Rais Mhe Samia Suluhu
- Awahakikishia usalama katika Kipindi chote cha Mkutano Mkuu wa Injili maarufu kwa jina la " Imani, Upendo, Miujiza "
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo Octoba 7, 2021 kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amefungua Mkutano Mkuu Injili maarufu kwa jina "Imani Upendo Miujiza"
Hafla ya uzinduzi huo imefanyika katika Hotel ya Hayatt Jijini Dar es Salaam.
Akitoa Salaam za Serikali Mhe Makalla amesema Rais *Mhe Samia Suluhu Hassan* anawaheshimu sana viongozi wa Dini na anathamini mchango wao katika mstakabali wa Taifa hili na leo alikuwa tayari kuja kufungua Mkutano huu Mkubwa wa Injili lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake ameshindwa kuhudhuria hapa leo.
Katika kudhihirisha imani yake na viongozi wa Dini hapa Nchini toka ashike kiti cha urais ndani ya miezi 6 tayari ameshakutana na makundi mbalimbali ya Viongozi wa Dini sote ni mashaidi Alisema Mhe Makalla
"Nchi sasa imetulia tuendelee Kumuombea Rais, Mama anatosha anaipeleka nchi pazuri katika Uchumi mzuri tumuombee agombee 2025 " Alisisitiza Mhe Makalla
Mkuu wa Mkoa amesema amefurahishwa na dhima ya Mkutano Mkuu wa Injili ambayo ni Kuliombea Taifa la Tanzania na Rais wake, tuendelee kuomba Amani, Upendo na Umoja ili Taifa lisonge mbele.
Mhe Makalla amebainisha kuwa yeye ni mwenyekiti wa Ulinzi na usalama DSM Mkutano huo Mkubwa wa Injili unafanyika DSM hivyo unabaraka zake zote.
Aidha Mhe Makalla amesema ni imani yake kuwa mikutano hiyo inafanyika huku kukiwa na taadhari kubwa dhidi ya Uviko - 19 na bahati nzuri kuna nguvu ya kimungu nyuma yake ambayo inaenda kuliweka Taifa la Tanzania katika Mikono Salama.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa