Wakati Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda akiwakarabisha Kundi la Madaktari Bingwa ambao ni Askari wa Kikosi cha Maji kutoka Jeshi la Jamhuri ya watu wa China nchini Tanzania ambao watakuja Tanzania na Meli kubwa ya Kikosi cha Wanamaji kutoka Jamhuri ya watu wa China wakiwa zaidi ya Wanajeshi na Madaktari 380 ikiwa ni Utekelezaji wa Kauli ya Balozi wa China aliyemaliza muda wake nchini, ambapo alimhakikishia Mhe Paul Makonda kuleta Timu ya Madaktari Bingwa watakaokuja kumsaidia katika juhudi zake za kutoa Huduma bora za Afya kwa Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wasiokuwa na kipato KIKUBWA cha kumudu gharama za matibabu.
Kutokana na Uwepo wa Madaktari hao, Mhe Paul Makonda ametangaza tena Kuanza kwa Zoezi jingine la kutoa Matibabu Bure, pamoja na vipimo BURE kwa Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam Kuanzia Tarehe 19 mpaka 25 mwezi huu (19-25/11/2017) matibabu ambayo yatatolewa Ndani ya Meli ya Kichina itakayoweka Nanga katika Bandari ya Dar es Salaam.
Pamoja na kutoa Matibabu Meli hiyo pia itatoa Huduma za upasuaji mdogo na mkubwa pamoja na kutoa dawa kwa watakaobainika kuitaji dawa, watakuja na baadhi ya vifaa vya kusaidia kutengeneza Mashine zetu za x -Ray na vipimo vingine ambazo ni mbovu katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Mhe. Paul Makonda amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika kuchangamkia FURSA ya Matibabu Bure kutoka China.
Katika hatua za awali za Utoaji wa matibabu Bure baadhi ya Watu wasiokuwa na Nia njema WALIBEZA jitihada za Mhe. Paul Makonda za Utoaji wa Huduma za Matibabu na upimaji BURE , lakini sasa Dunia imetambua na kuamua kumuunga mkono katika Juhudi zake za kuhakikisha wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wanapata huduma bora za Afya kwa Gharama nafuu
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa