Mhe Amos Makalla akikagua barabara ya Makongo Juu - Goba inayojengwa kwa kiwango cha lami.
- Amtaka mkandarasi wa Barabara hiyo kujitathimini
- Ameagiza ifikapo Octoba 8, 2021 barabara iwe imekamilika
- Atembelea miradi ya Maji DAWASA inayotekelezwa yenye thamani zaidi ya bilioni 65
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo Agosti 27,2021 ametembelea mradi wa *barabara Mkongo Juu wenye urefu wa KM 4.5 na miradi ya maji eneo la Makongo, Tegeta A na Mbweni
Akiwa katika ukaguzi wa barabara ya Makongo kuelekea Goba amesema ajaridhiswa hata kidogo na kasi ya utendaji kazi wa Mkandarasi, amemuagiza Meneja wa TANROAD Mkoa wa Dar es Salaam kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa mradi huo, ukamilike kwa wakati ili wananchi waweze kutumia barabara hiyo kama ilivyo kusudiwa.
Mhe Mkuu wa Mkoa amemtaka Mkandarasi huyo kujitathimini kwa kuwa hata leo akiwa katika eneo la tukio amekuta vifaa vichache vya kazi hali ambayo imemkatisha matumaini ya kuisha kwa wakati kama hata jirekebisha ndipo akaagiza amechoka kusikia malalamiko ya barabara hiyo ifikapo Octoba 8,2021 barabara iwe imekamilika.
Kwa upande wa Mhandisi wa TAN ROAD Mkoa *Mwanaisha Rajabu* amekiri kupokea maagizo ya Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya utekelezaji.
Aidha Mhe Makalla ametembelea miradi ya maji DAWASA inayotekelezwa katika eneo la Tegeta A Goba na Mbweni ambayo kukamilika kwake itagharimu zaidi ya bilioni 65
Mhe Makalla ameridhishwa na ujenzi wa matenki hayo makubwa ambapo amesema ni suluhisho la kero ya siku nyingi ya maji maeneo ya pembezoni kama, Mivumoni, mbweni, Bunju, Kinzudi, Salasala, na Mabwepande.
" Niwatake DAWASA kukamilisha mradi hiyo kwa wakati na chunguzeni kwa makini ubora wa mabomba mnayotandaza chini ili mabomba hayo yakae kwa muda mrefu " Alisema Mhe Makalla
Mhe Amos Makalla akitoa maagizo katika mradi wa maji eneo la Tegeta A Goba unaotekelezwa na DAWASA mapema leo.
Ifahamike kuwa ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa aliyoifanya akianzia na maradi barabara ya Mkongo juu Goba, miradi ya ujenzi wa Matenki makubwa ya maji Tegeta A Goba, na Mbweni itakapokamilika itachochea shughuli za uchumi kwa upande wa barbara na kuwaondolea wananchi na wakazi kero na adha ya upatikanaji wa maji Jijini Dar es Salaam.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa