Wafanyakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam waungana na Wafanyakazi wenzao Duniani kuadhimisha sherehe za Mei Mosi ambapo Kimkoa zimefanyika katika Uwanja wa Uhuru.
Sherehe hizo zilianza kwa maandamano ya wafanyakazi hao yaliyoanzia TUCTA Makao Makuu, Mnazi Mmoja kuelekea katika Uwanja wa Uhuru ambapo yalipokelewa na mgeni rasmi Mhe. Magreth Sitta (Mb).
Sherehe za mwaka huu zinaongozwa na kauli mbiu isemayo "UCHUMI WA VIWANDA UZINGATIE HAKI, MASLAHI NA HESHIMA YA WAFANYAKAZI". Kauli mbiu hii inazingatia utu wa wafanyakazi hasa katika kipindi hiki tunachoelekea katika mabadiliko makubwa ya uchumi wa viwanda dhana ambayo Tanzania ya viwanda inatuelekeza kuwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa