Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo April 09, 2024 amedhihirisha kwa vitendo uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia uzinduzi wa kampeni kabambe ya kuelimisha umma kanda ya pwani kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa minara 758 ya Mawasiliano ya maeneo ya vijijini na machache ya mjini.
Uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa JNICC Dar es Salaam lakini kampeni hiyo itaendelea katika mikoa yote ya Kanda ya pwani ambapo lengo la kampeni ni kuhakikisha inatolewa elimu kwa viongozi wote wa Mkoa waweze kuisemea vema Serikali katika utekelezaji wa mradi huo kwa wananchi na namna Serikali ya awamu ya sita inavyotekeleza masuala ya mawasiliano bila kubagua mtanzania yoyote.
Aidha RC Chalamila amesema leo mfuko wa mawasiliano kwa wote UCSAF umewaita hapa viongozi mnaowawakilisha watanzania katika maeneo yenu mpate elimu ili nanyi mkazisambaze kwa wananchi katika maeneo yenu ya kiutendaji.
Vilevile RC Chalamila amesema mradi wa ujenzi wa minara 758 ya mawasiliano wenye thamani ya Bilioni 126 Serikali imeshafanya malipo ya awali fedha kiasi cha Bilioni 64,5357,200 kwa wakandarasi wote.
Mradi huu unalenga kufikisha huduma za mawasiliano ya simu (sauti, intanet/Data) katika Kata 713 ambapo minara 758 itajengwa na makampuni ya simu ikiwemo TTCL, VODACOM, AIRTEL, HALOTEL NA TIGO
Hadi sasa Serikali kupitia UCSAF imeshaingia mikataba na watoa huduma za mawasiliano kufikisha huduma katika Kata 1974 zenye vijiji 5111 kwa kujenga jumla ya minara 2158 ambapo minara hii ikikamilika wananchi takribani 23,798,848 watapata huduma hiyo ya mawasiliano ya simu kwa uhakika.
Mwisho hadi sasa jumla ya Kata 1306 zenye vijiji 3838 na wakazi 16,084,834 wameshafikiwa na huduma ya mawasiliano kwa jumla ya minara 1432 iliyojengwa tayari katika kata hizo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa