- Ujumbe wa Wataalamu hao Umelenga kuboresha Sekta ya Afya Katika Mkoa wa Dar es Salaam
- Kuwaongezea uwezo wataalam katika Sekta ya Afya ndani ya Mkoa
- Kuimarisha mifumo ya maabara katika hospitali za Mkoa na Vifaa tiba
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndg Hassan Abbas Rugwa amepokea ujumbe wa Wataalam wa Afya Kutoka Italy leo Septemba 7,2021 Ofisini kwake Ilala Boma, Dar es Salaam
Ujumbe huo ukiongozwa na Balozi wa Italia nchini Tanzania Mhe Marco Lambard, Dkt Beatrice Borchi na Ms Giulia Dagliana wote kutoka Kituo chaTaifa la Italia cha Afya Duniani.
Kwa upande wa Tanzania walioambatana na ujumbe wa wataam hao ni Dkt Fadhili Kibaya Ofisa kutoka Wizara ya Afya na Ndg Mohamed Mohamed Ofisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje.
Katibu Tawala wa Mkoa Ndg Hassan Rugwa alipata wasaa wa kufanya mazungumzo na wataalam hao ambapo lengo hasa la kutembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ni kuona namna ya kuweza kuboresha Sekta ya afya katika Mkoa.
Wataalam hao wamebainisha maeneo ambayo watasaidia kuboresha ni kama Kuwajengea uwezo wataalam wa Afya, Kuboresha mifumo ya Maabara katika hospitali, Vifaa tiba na Gari la wagonjwa "Ambulance"
Aidha wataalam wa Afya kutoka Italia wamebanisha dhamira yao ya kushirikiana na Mkoa katika kutoa elimu na kuhamasisha jamii juu ya Umuhimu wa chanjo ya UVIKO-19
Vilevile Ujio wa ujumbe huo wa Wataalam wa Afya kutoka Italia ni kielelezo cha kukuza mahusiano na kuendeleza ushirikiano katika Sekta ya Afya kati ya Tanzania na Italia
Ifahamike kuwa Taifa la Italia limetenga Euro 1,250,000 ikiwa ni Msaada wenye manufaa kwa Tanzania hivyo lengo la ujio wa Wataalam hao ni kuweza kubainisha *mahitaji na Vipaumbele vitakavyoweza kufadhiliwa kwa fedha hizo katika Sekta ya Afya.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa