Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo ametembelea na kukagua Hospital ya kisasa ya Mama na Mtoto iliyojengwa Chanika ambayo ujenzi wake umekamilika.
Uwepo wa Hospital hiyo yenye viwango vya kisasa ni matokeo ya juhudi za Mheshimiwa Paul Makonda baada ya kuwatafuta wafadhili ambao ni Serikali ya Korea Kusini chini ya Shirika la KOICA.
Hospital hiyo itakuwa na uwezo wa kuchukuwa Vitanda 160 ambapo ndani yake kuna Vyumba vya kutosha vya Upasuaji, Maabara, Madaktari, Sindano, ICU, Wodi za Wajawazito na Watoto pamoja Nyumba za Watumishi.
Mhe. Makonda amesema Hospital hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto za Afya kwa wakazi wa Chanika ambao walikuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata huduma Amana na wakati mwingine kinamana walikuwa wakijifungulia Njiani na wengine kupeteza Maisha.
Amewataka wauguzi kuhakikisha wanatoa huduma bora za Afya kwa Wagonjwa kwa kuepuka kuwatolea Wagonjwa lugha Chafu ilikuhakikisha Wananchi hawapati usumbufu wowote.
Katika hatua nyingine Mhe. Paul Makonda amesema kuwa amefanikiwa kupata mtu atakayetoa Mkopo wa Viwanja bila masharti magumu kwa watumishi ikiwemo Walimu, Askari,Wauguzi na Madakrari ilikuboresha Maisha yao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa