# Aipongeza Wilaya ya Ilala kwa kutatua KERO za wananchi wake
# Asisitiza kukaa mpaka usiku katika kutatua KERO za wananchi MAJIMBONI
# Aahidi Kumleta Mhe. Rais katika uzinduzi wa Machinjio ya Kisasa
# Aendelea kuomba wananchi kudumisha Ulinzi na Usalama katika maeneo yao.
# Akerwa na Uuzwaji wa Biashara Holela Mashuleni, Barabarani na Katika njia za watembea kwa miguu
# Awaelekeza DAWASA kuweka kambi Buguruni ili kuondoa changamoto ya maji taka
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla leo tarehe 1 Septemba ameendelea na ziara yake katika Wilaya ya Ilala Jimbo la Segerea.
Akiwa katika Jimbo Hilo Mhe.Mkuu wa Mkoa ameipongeza Wilaya hiyo kwa kupokea KERO chache kutoka kwa umati Mkubwa wa wananchi waliokuwepo ukilinganisha na Majimbo mengine aliyoyapitia.
Amesema " Ukiona uchache huo wa KERO za wananchi ujue Viongozi wake wanafanya kazi kubwa ya kutatua KERO zao vizuri" RC Makalla
Mhe. Makalla amesema kuwa katika Jimbo la Kawe alisikiliza na kutatua KERO za wananchi mpaka saa 11:00 Jioni aidha katika Jimbo la Kibamba alisikiliza na kutatua KERO za wananchi mpaka saa 1:00 Usiku
Awali Mkuu wa Mkoa alipokea KERO kutoka katika Jimbo hilo kuwa ni pamoja na Kero ya Barabara, Matatizo ya Urasimishaji, Matatizo ya Maji, Migogoro ya Ardhi, Malipo ya Fidia, Bonde la Mto Msimbazi, na Stendi ya Mabasi ya Muhimbili
Kuhusu uzinduzi wa Mradi Mkubwa wa Machinjio ya Kisasa ya Vingunguti uliotumia gharama ya shilingi *billioni 38* Mhe. Makalla ameahidi Kumleta Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuja na kuzindua Mradi huo kwani umekamilika kwa sasa, Mradi Mkubwa na unaenda kuifungua Dar es Salaam Kimataifa.
Wakati huo huo Mhe. Mkuu wa Mkoa ameendelea kuwaomba wananchi kudumisha Amani na Utulivu uliopo katika maeneo yao kwa kuwafichua wahalifu wote endapo wataonekana kuwepo katika maeneo yao.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amesema amekua akikerwa na Uuzwaji wa Biashara Holela Mashuleni, Barabarani, na katika njia za watembea kwa miguu kwani wanahatarisha Usalama wa watu kwa ujumla kwa kufanya Biashara maeneo hatarishi.
Kwa upande wa KERO ya majitaka yanayotiririka katika baadhi ya maeneo ya wakazi wa Buguruni Mhe. Mkuu wa Mkoa amewataka DAWASA kuweka kambi Buguruni ili kuondoa KERO hiyo
Serikali ya Awamu ya Sita kupitia Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan imeahidi kuukamilisha miradi yote iliyoanza kutekelezwa hivyo Awamu hii ya tatu ya DMDP tayari Billioni 3.8 zimeshatengwa ili kujenga Barabara katika Wilaya ya Ilala alisema Mhe. Amos Makalla
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa