Baadhi ya wananchi wakisubiri kuwasilisha kero zao katika uwanja wa Tanganyika Perkers Jimbo la Kawe mapema leo.
- Wananchi wengi wajitokeza,kuelezea kero zao na kutatuliwa papo hapo
-Atembea na Wataalamu wa Idara zote kutoka Sekretarieti ya Mkoa, Manispaa ya Kinondoni, LATRA na POLISI
Aahidi kwenda na Waziri wa Ardhi na Kamishna- Mabwepande
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla Leo tarehe 30 Agosti, 2021 ameanza ziara rasmi ya kupita Jimbo kwa Jimbo katika Mkoa huo ili kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua papo kwa papo.
Mhe. Makalla ameanza na Jimbo la Kawe lililopo katika Wilaya ya Kinondoni ili kuwafuata wananchi waliopo pembezoni ambapo ndipo kwenye changamoto nyingi.
Akiwa katika Jimbo hilo Mhe. Mkuu wa Mkoa alishuhudia umati Mkubwa wa wananchi uliofika mahali hapo ili kutatuliwa KERO zao.
Mhe. Mkuu wa Mkoa alipokea KERO mbalimbali zinazohusu Ubovu wa Barabara, Migogoro ya Ardhi, Mafuriko,Ukosefu wa maji katika baadhi ya kata,wananchi kubomolewa nyumba zao bila utaratibu, Ukosefu wa shule kwenye baadhi ya maeneo , dhuluma ya Fedha za watu katika ununuzi wa Viwanja, Kelele za Baa na ucheleweshwaji wa upatikanaji wa Ajira.
Mhe. Makalla kupitia Wataalamu wake wa Mkoa, Manispaa, LATRA, POLISI alihakikisha wananchi wote walioleta KERO zao wamepatiwa MAJIBU ya papo kwa papo na yale yaliyohitaji kufanyiwa kazi yapatiwe majibu ifikapo tarehe 6 Septemba, 2021.
Awali Mhe Amos Makalla alieleza kuwa Manispaa ya Kinondoni Migogoro Mikubwa sana ni ya Ardhi ambapo ameshuhudia eneo la Mabwepande ndipo penye Migogoro mingi hivyo kuahidi kwenda na Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi na Kamishna Ili kutatua KERO za huko.
Mhe. Mkuu wa Mkoa amewaambia wananchi wa Kawe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anatambua uwepo wa ziara hii na amesema KAZI IENDELEE aidha amepongeza uwepo wa miradi mbalimbali iinayoendelea katika Jimbo hilo na kusisitiza utolewaji wa taarifa kwa ngazi husika kabla ya utekelezaji wa Mradi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa