Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda mapema leo alfajiri amefika kituo cha Mabasi ya Mwendokasi Kimara kujionea mwenyewe adha wanayoipata abiria ambapo amewaomba abiria kuwa watulivu wakati Serikali ikiendelea kushughulikia kasoro zote.
Miongoni mwa kero alizojionea RC Makonda ni uchache wa mabasi, Msongamano wa watu unaoweza kusababisha kuenea kwa magonjwa, kukosekana kwa usawa kwa makundi maalumu ikiwemo Wazee, Walemavu na Wajawazito kusafiri, abiria kugombea magari na kuumizana, wizi, msururu wakati wa kukata Tiketi na baadhi ya magari kuacha abiria vituoni.
RC Makonda ameagiza Polisi kuwakamatwa madereva wote wanao park magari badala ya kutoa huduma jambo linalosababisha usumbufu kwa abiria.
Aidha RC Makonda amewaruhusu wananchi wanaonyanyaswa na watoa huduma kuwapiga picha ili ifikie hatua pasiwepo na unyanyasaji wa aina yoyote kwa abiria.
Pamoja na hayo RC Makonda amempongeza Waziri wa TAMISEMI kwa kuchukuwa hatua za haraka kwa kuagiza watendaji kumaliza changamoto zinazokabili usafiri huo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa