Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo ametembelea na kukagua Ukarabati wa Magari 26 ya Polisi yaliyopelekwa Mkoani Kilimanjaro yakiwa Mabovu kwa ajili ya kukarabatiwa na kubadilishwa mwonekano ambapo hadi sasa Magari 18 yapo hatua ya mwisho kukamilika.
Magari hayo ambayo yalipelekwa Kilimanjaro yakiwa chakavu kwa sasa baadhi yanatembea ambapo yamepakwa rangi huku yakifungwa vifaa mbalimbali ikiwemo Magurudumu Mapya, Taa, Vioo, Bodi, Side Mirrow na vifaa vingine muhimu.
Mhe. Makonda amesema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa na kusema kuwa atakabidhiwa magari hayo mwanzoni mwa mwezi October ili ayakabidhi kwa Jeshi la Polisi.
Amesema Magari hayo yenye mwonekano kama yale ya UN yatakuwa na uwezo wa kubeba Askari Tisa nyuma wakiwa wamekaa ambapo Watatu watakuwa wakitazama Nyuma, Watatu Kushoto, Watatu Kulia na Mmoja Mbele wote wakiwa wamebeba silaha.
Aidha Mhe. Makonda amesema kupatikana kwa Magari hayo yatasaidia kupunguza vitendo vya uhalifu kwa wananchi.
RC Makonda amesema kuwa lengo lake ni kuona hakuna Mwananchi yoyote anayeibiwa au kuporwa kitu.
Hata hivyo amesema baadhi ya askari walikuwa wakipoteza maisha na kuporwa Silaha kutokana na aina ya magari waliyokuwa wakitumia kutowapa uwezo wa kukabiliana na wahalifu hivyo magari hayo yatamaliza matukio hayo.
Ameishukuru kampuni ya RSA Limited kwa kumuunga mkono kwa kujitolea kukarabati Magari 56 ya Jeshi la Polisi kwa kuyafanya kuwa ya kisasa na Mapya.
Sanjari na hayo amesema Magari hayo yataenda kufanya Doria kwa masaa 24.
Nae Mkurugenzi wa Kampuni ya RSA Bwana Manmohan Bhamra amesema kwa sasa Magari hayo ni sawa na Mapya kwakuwa yamewekwa vifaa vipya.
Amesema Magari yote watayakabidhi kwa wakati iliyakaongeze tija katika kuimarisha Ulinzi na Usalama kwa Wananchi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa