Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo amekagua ujenzi wa Jengo la Huduma ya Dharura kwenye Hospital ya Rufaa Temeke ambayo Ujenzi wake unafadhiliwa na Ubalozi wa Japan Nchini Tanzania
Ujenzi wa Jengo hilo unagharimu kiasi cha Shillingi Million 800 ambazo ni matunda ya jitiada binafsi za Mhe. Makonda baada ya kumtafuta Balozi wa Japan Nchini Tanzania na kumueleza changamoto ya ukosefu wa kitengo cha Huduma za haraka kwenye Hospital za Mkoa ambapo baada ya mazungumzo Balozi alipokea kwa mikono miwili ombi la RC Makonda.
Mhe. Makonda amesema kukamilika kwa jengo hilo kutasaidia kupunguza Vifo vitokanavyo na wagonjwa wanaohitaji huduma ya haraka na kuikosa huduma hiyo kwa uharaka.
Amesema jengo hilo ni mahususi kwa ajili ya wagonjwa wote wanaohitaji huduma ya haraka hususani majeruhi wa ajali, wanaougua Malaria kali ya ghafla, maumivu ya tumbo, wanaobanwa na Kifua, Wajawazito, Homa kali, ajali ya Moto na magonjwa yote yanayohitaji huduma ya haraka.
Amebainisha kuwa wagonjwa wanaohitaji huduma ya haraka wanaofikishwa Hospitalini hapo wamekuwa wakipelekwa Hospital ya Muhimbili ambako ni mbali kutoka Temeke hivyo kusababisha wengi wao kupoteza maisha Barabarani.
Aidha Mhe. Makonda amesema baada ya kumalizika kwa jengo hilo ujenzi wa majengo ya huduma ya haraka utahamia kwenye Hospital ya Amana na Mwananyamala ili kuipungizia mzigo Muhimbili
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Temeke Dr. Aman Malima amesema kwa siku wanapokea wagonjwa kati ya 1,800 -2,000 ambapo kati ya hao 200 ni wagonjwa wanaohitaji huduma ya dharura hivyo amesema uwepo wa huduma hiyo utasaidia kuokoa maisha.
Amempongeza Mhe. Makonda kwa juhudi zake binafsi za kutafuta wadau waliofanikisha ujenzi wa Jengo hilo.
Nae mkandarasi wa ujenzi huo Bwana Abdulkadir Msangi amesema ujenzi umefikia 85% ambapo hadi kufikia mwishoni mwa mwezi wa Novemba ujenzi utakuwa umekamilika na jengo kukabidhiwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa