Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa PAUL MAKONDA leo amefanya Ziara ya kukagua miundombinu iliyoathiriwa na Mafuriko yaliyotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha na kusema Serikali itakarabati mara moja miundombinu yote iliyoathiriwa na Mvua.
Katika ziara hiyo RC MAKONDA ameambatana na Kamati ya Maafa ya Mkoa ambapo wametembelea maeneo mbalimbali yaliyoathiriwa na Mvua ikiwemo Jangwani, Daraja la Malecela, Daraja la Korongo, Daraja la Tandale kwa Mtogore, Africana na Boko Basihaya na kutoa pole kwa Wahanga.
Akizungumza na Wananchi hao RC MAKONDA amewataka Wananchi waliojenga kwenye maeneo hatarishi kuchukuwa tahadhari mapema kwakuwa Wataalamu wa hali ya Hewa wametangaza kuwa Mvua kubwa zitaendelea kunyesha.
Amesema kuwa Ujenzi wa Miundombinu iliyoharibiwa ikiwemo ya Maji, Umeme, Mitaro, Barabara na Madaraja inaendelea ambapo kwenye Daraja la Malecela ameagiza kujengwa Daraja la Muda mfupi chini ya Vijana kutoka Jeshi la Wananchi.
RC MAKONDA amesema kuwa zaidi ya Shilingi Billion Moja zimetolewa na Bank ya Dunia kwa ajili ya Maboresho ya eneo la Jangwani ambapo amesema Serikali ya Mkoa ina vifaa vya kutosha kwa ajili ya kuokoa Wananchi.
Aidha RC MAKONDA amesema kuwa miongoni mwa sababu zilizopelekea Maji ya mvua kukosa mwelekeo ni Ujenzi holela, Uchimbaji wa Mchanga na watu kutupa Uchafu kwenye Mito.
Miongoni mwa Wilaya alizotembelea RC MAKONDA ni pamoja na Ilala, Ubungo na Kinondoni ambapo kuna nyumba zaidi ya 200 zipo kwenye mazingira hatarishi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa