Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ameunda kamati ya watu 17 watakaofanya operesheni kabambe ya kuwafundisha adabu watu wanaofanya ushoga, nyumba zinazotumika kurekodi video za Ngono, wanaojiuza na matapeli wa njia ya mitandao.
RC Makonda amesema kamati hiyo inajumuisha maafisa wa Polis, TCRA, Wanasheria, Bodi ya Filamu, Madaktari na Wataalamu wa ushauri na Nasaaha ambapo kamati hiyo itaanza zoezi la kamatakamata jumatatu.
Operesheni hiyo imepokelewa kwa mikono miwili na mamilioni ya wananchi ambao wamekuwa wakichukizwa na mmomonyoko wa maadili ambapo RC Makonda hadi sasa amepokea Meseji (Jumbe) zaidi ya 18,000 za watu wanaopongeza na kutaja majina ya watu wanaofanya matendo maovu ikiwemo ushoga na biashara ya ngono.
Aidha RC Makonda amesema hadi sasa amepokea majina zaidi ya 200 ya mashoga waliotajwa wakiwemo kina James Delicious, Dida Mtamu, Abas, Aunt Miliki na kundi la Pachupachu.
Pamoja na hayo RC Makonda amesema oparesheni hiyo pia itahusisha sehemu za Masaji ambazo baaadhi yake zimekuwa zikijihusisha na biashara ya ngono.
Hata hivyo RC Makonda amesema kuwa hata wanaume watakaotajwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi (wateja) wa Mashoga watakamatwa na kuchukuliwa hatua Kali za kisheria kwa mujibu wa Sheria.
Sanjari na hayo RC Makonda ametoa angalizo kwa watu wenye picha na video za ngono kwenye simu zao kuwa operesheni hii haitowaacha salama.
WAZAZI TUSHIRIKIANE KUPINGA USHOGA NA BIASHARA YA NGONO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa