Mkoa wa Dar es Salaam ameadhimisha Siku ya Uhuru kwa Kuwatembelea Wafungwa na Maabusu kisha kupata Chakula cha Pamoja na kutoa huduma ya Masaada wa Kisheria na Ushauri Nasaha kwa Wafungwa na Mahabusu.
Katika Maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. PAUL MAKONDA ametoa Msaada wa Runinga za Kisasa 69 (Flat Screen) Touch zenye ukubwa wa Inch 40 kwa Magereza na Hospitali zote za Mkoa wa Dar es Salaam ili kuwawezesha Wafungwa na Wagonjwa kupata haki ya kikatiba ya kupata Habari.
Hii ni Historia kwa Dar es salaam kuwa Mkoa wa kipekee wenye Runinga Magerezani zinazowawezesha Wafungwa na Mahabusu kupata Habari na Hotuba za Rais ili kuwapunguzia Msongo wa Mawazo ili wasiwe na Mawazo ya kujiua ambapo zitagawanywa kwenye Magereza ya Segerea, Keko na Ukonga.
RC MAKONDA aliongozana na Viongozi wa Dini waliowafariji Wafungwa na Kuwafanyia Sala na Dua huku Watu wa Ustawi wa Jamii wakitoa Msaada wa Ushauri Nasaha kwa Wafungwa.
RC MAKONDA ambae amepokelewa kwa Furaha kubwa na Wafungwa wa Gereza hilo amewasihi kutokata tamaa kwa kuwa bado wanayo nafasi ya kutimiza ndoto zao baada ya kumaliza kifungo ambapo amewahimiza kuwa Mabalozi Wazuri kwa Jamii.
Ili kupunguza msongamano wa Mahabusu Gerezani RC MAKONDA amesaidia zaidi ya Mahabusu na Wafungwa 200 wa Gereza la Segerea kupata Msaada wa Sheria ambao walikuwa hawana uwezo kifedha.
Aidha RC MAKONDA ametoa Magodoro 100, Vifaa vya Usafi na Sabuni za Kuoga na Kufua kwa Wafungwa na Mahabusu.
Baadhi ya Mahabusu na Wafungwa wamemshukuru RC MAKONDA kwa kuwa kiongozi wa Kwanza na wa pekee aliewatembelea na kupata chakula cha pamoja, kuwapatia Runinga, kusikiliza changamoto zao na kuwapatia Wanasheria na watu wa Ustawi wa Jamii kitendo kilichowafariji.
Aidha Wameshukuru pia kitendo cha RC MAKONDA kusikiliza changamoto zao na kuzipatia majibu ambapo wamemuahidi kuwa wamebadilika na watakuwa mabalozi wazuri kuhimiza jamii kuzingatia Sheria.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa