Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ameahidi kuwapatia shilingi milioni 10 chama cha wajane Tanzania kama sehemu ya sadaka yake ya Jumapili ili kuhakikisha wajane wanapata ofisi ya kudumu ya kushughulikia mambo yao.
Kutokana na hilo RC Makonda amewaagiza Wakuu wa Wilaya kutafuta eneo maalumu ambalo litafaa kujenga ofisi za kisasa za Makao Makuu ya Chama cha wajane.
Hatua ya RC Makonda kutoa ahadi hiyo ni baada ya kusikia kilio cha wajane ambao wameeleza kuwa wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa ofisi ya kudumu jambo linalowalazimu kufanya shughuli zao katika jengo la Kukodi na wakati mwingine wanakosa fedha za kulipia kodi ya pango.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa