Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda leo amewahimiza Wananchi wote waliojenga kwenye maeneo hatarishi ikiwemo mabonde na sehemu zenye miinuko kuondoka ili kujikinga na uharibifu wa Mali na vifo visivyokuwa na ulazima.
RC Makonda ametoa kauli hiyo leo wakati alipofanya ziara ya kukagua uharibifu wa nyumba zilizovunjika eneo la Kingugi kwa Mnyani Kata ya Kilungule baada ya wakazi kujenga kwenye maeneo yasiyoruhusiwa.
Aidha RC Makonda amewaagiza Wenyeviti wote wa mitaa kuainisha nyumba zilizojengwa kwenye maeneo hatarishi ambapo amewataka kutoruhisu watu kujenga maeneo ya mabondeni.
Katika kutafuta mwarobaini wa tatizo la wananchi waishio mabondeni RC Makonda ameandaa mkutano wa wananchi wote waishio maeneo ya mabondeni kwa ajili suluhisho la kudumu.
Katika ziara alizofanya RC Makonda amejionea nyumba nyingi zikiwa zimejengwa kwenye maeneo yasiyo rasmi kiasi kwamba hata ikitokea janga la moto inakuwa vigumu Jeshi la zimamoto na uokoaji kufika na hata mgonjwa akizidiwa ghafla ni vigumu kuwahishwa hospitali jambo ambalo ni hatari kwa usalama.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa