Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda anawaalika vijana wote wenye utaalamu wa Teknolojia yani IT kufika Ofisini kwake Tar 01/11/2018 Asubuhi kwa ajili ya kuunda Mfumo wa kuratibu Uwajibikaji wa Watendaji wa Umma ilikuhakikisha kero na malalamiko ya wananchi yanashughulikiwa kwa uharaka.
Mfumo huo utakuwa ukipokea malalamiko ya watendaji wasiowajibika kuanzia ngazi ya Mitaa, Kata, Wilaya, Mkoa na viongozi Wakuu akiwemo Mkuu wa mkoa, Katibu tawala Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Makatibu tawala wilaya na wakuu wa idara Watakuwa wakiona ni mtendaji gani asiewajibika kutatua kero za wananchi.
RC Makonda amesema hataki kuona wananchi wanafika kwenye ofisi za umma na kuambiwa "Njoo kesho" kila siku pasipokujua kuwa wanatumia nauli na kupoteza muda.
Mfumo utampa mwananchi uwezo wa kueleza malalamiko yake endapo amefika ofisi ya umma na watendaji kushindwa kushughulikia kero zake kwa uzembe.
SHAUKU YA RC MAKONDA NI KUONA UWAJIBIKAJI NA UTENDAJI KWENYE OFISI ZA UMMA UNAONGEZEKA ILI KUPUNGUZA KERO KWA WANANCHI.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa