Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo Julai 11 ametangaza Shindano litakakalohusisha Watu wote wanaoendesha Platform za Social Media ikiwemo Waandishi wa habari Blog, Website, Online Tv, Instagram, Twitter, Facebook na nyinginezo ambapo watakuwa na jukumu la kuuliza wananchi maswali kuhusu Jumuiya ya Nchi za SADC ambapo washindi wa shindano hilo watajishindia kitita cha mamilioni ya Fedha.
RC Makonda amesema utaratibu wa kushiriki Shindano hilo ni Wahusika kwende kwenye sehemu za Bar, Saloon, Vijiwe vya bodaboda na Sokoni kisha kuwahoji wananchi waeleze namna wanavyoifahamu jumuiya ya SADC na kurusha mahojiano hayo kwenye platform zao ambapo pia wananchi watakaoweza kutoa majibu kwa ufasaha nao watapatiwa kiasi cha shilingi Laki moja.
Aidha RC Makonda amesema Mshindi wa kwanza wa shindano hilo atapatiwa kiasi cha Shilingi Milioni 3, Mshindi wa pili Milioni 2 na Mshindi wa tatu Milioni 1 ambapo hafla ya kukabidhi zawadi hizo itafanyika August 05 mwaka huu.
Hata hivyo RC Makonda amewataka Wamiliki wa Platform za Social Network kudhihirishia jamii kuwa mitandao yao ina uwezo mkubwa wa kubadilisha jamii kama ikitumika vizuri ambapo kwa kufanya hivyo watazidi kuheshimika na pia kuingiza pesa kupitia matangazo.
Huu ni mkakati wa RC Makonda kuendelea kuboresha maisha ya vijana waliojiajiri na kuajiri wenzao kupitia mitandao ya kijamii akiamini kupitia mitandao hiyo wanaweza kupata kipato kikubwa na serikali ikapato kodi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa