Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewataka Vijana waliomaliza mafunzo ya JKT na Mgambo na hawana kazi kufika ofisini kwake Ijumaa ya July 06 kwa ajili ya kupatiwa ajira ya kusimamia usafi na kuwatoza faini vinara wa uchafuzi wa mazingira.
RC Makonda amesema katika fedha itakayotozwa kwa wachafuzi wa mazingia 50% itaenda kwenye Halmashauri na 50% kwa vijana wa JKT na Mgambo ambapo kabla Vijana hao hawajakabidhiwa jukumu hilo watapewa mafunzo ya Sheria ya Usafi.
Huu ni Ubunifu Mkubwa aliofanya RC Makonda katika kutatua tatizo la ajira kwa vijana sambamba na kuufanya mji kuwa katika hali ya usafi baada ya mbinu nyingi zilizokuwa zikitumiwa kuhamasisha usafi kutokuwa na matokeo mazuri.
Aidha RC Makonda ameagiza makampuni yote yaliyopewa tenda ya usafi Dar es salaam kuanzia ngazi ya Mitaa, Kata na Halmashauri kufika ofisini kwake Jumatano ya July 04 wakiwa na mikataba yao kwa ajili ya kujiridhisha uwezo wao wa kufanya kazi baada ya uchunguzi aliofanya kubaini uwepo wa kampuni zilizopewa tenda Kubwa wakati hawana vifaa vya kutosha.
Hata hivyo RC Makonda ameziagiza Manispaa zote za Jiji hilo kuhakikisha kila mfanyabiashara na vituo vya daladala vinakuwa na Sehemu ya kuweka taka (dustbin).
Pamoja na hayo RC Makonda ametangaza fursa kwa wadau wenye vyoo vya kuhama (mobile toilet) kufika ofisini kwake ili wakutanishwe na Halmashauri ili waweke makubaliano ya ushirikiano ili kuondoa tabia ya watu kujisaidia kwenye kuta na vichochoro.
Miongoni mwa majukumu ya Vijana hao ni kuhakiki makampuni kwenye mitaa kama yapo na yanafanya kazi kweli, kujua wananchi wanapeleka wapi takataka, kukamata watupaji wa taka na kuwatoza faini ambapo Kama huna pesa utapewa adhabu ya kufanya usafi wiki nzima chini ya usimamizi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa