Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa huo Kuunda Timu ya kufanya ukaguzi wa Mali zote za Serikali zilizotaifishwa na wajanja ikiwemo maeneo ya wazi, Nyumba za umma na kubainisha mikataba yote mibovu inayoinyonya Serikali.
RC Makonda ametoa agizo hilo leo wakati wa hafla ya kuwakaribisha wakuu wapya wa wilaya za Kinondoni na Kigamboni, Katibu Tawala Mkoa na kuwaaga wakuu wa wilaya waliohamishwa vituo vya kazi ambapo amemuagiza katibu tawala kuhakikisha anakamilisha ripoti kabla ya September 03 mwaka huu.
Aidha RC Makonda amewataka watendaji kuhakikisha wanasimamia ipasavyo suala la ukusanyaji wa mapato na kuangalia chanzo kilichopelekea Mkoa huo kutofanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato pamoja na kufanyia kazi kasoro zilizojitokeza.
Pamoja na hayo RC Makonda amemtaka Katibu Tawala kupanga safu mpya ya utendaji kazi ili kuhakikisha wanatatua kero za wananchi ambapo ametaka kuanza na Idara ya Ardhi, Biashara, Usafi, Mapato na Michezo ambazo bado hazijamridhisha kiutendaji kazi.
Hata hivyo RC Makonda amewasihi viongozi walioteuliwa kuchapa kazi ili kuenda sambamba na kasi ya Rais Dkt.John Magufuli aliewaamini na kuwateua
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa