Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amesema zoezi la kuwakamata wazururaji katika mkoa huo limeanza rasmi leo ambapo wazururaji watakaokamatwa watapewa adhabu mbalimbali ikiwemo Kusafisha mitaro, Kusafisha barabara, kufyeka nyasi na kulima bustani.
RC Makonda amesema kama kuna watu walidhani watapelekwa mahabusu na kula Chakula cha bure wasahau kabisa jambo hilo.
Mhe. Makonda ametoa kauli hiyo wakati wa Uzinduzi wa Shoppers Supermarket ya Mlimani City ambapo ameonyesha kufurahishwa na uwekezaji uliofanyika na wazawa jambo lililosaidia zaidi ya Vijana 205 kupata Ajira kwa Shoppers ya Mliman City pekee.
Aidha RC Makonda amesema uwepo wa Supermarket hiyo licha ya kuwezesha wananchi kupata mahitaji muhimu pia serikali inapata Kodi ambapo inaelezwa kwa kipindi cha miezi nane pekee ambayo Jengo hilo kikifungwa serikali ilikosa kodi ya shilingi Bilioni 28.
Pamoja na hayo RC Makonda amesema uwepo wa Supermarket hiyo pia utawezesha Wafugaji na Wakulima wa Mazao ya Matunda na Mbogamboga kupata sehemu ya kuuza Mazao yao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa