Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amekabidhi hati ya nyumba kwa familia ya Bi. Zainabu Kaswaka iliyoteseka na kusababisha ugonjwa wa Kupooza kwa Mume wake baada ya nyumba na ardhi yao kuuzwa baada ya Matapeli kutumia hati ya nyumba yao kuchukuwa mkopo Benki ya FNB pasipo familia kujua.
Upatikanaji wa hati hiyo umekuja baada ya majadiliano ya kina baina ya RC Makonda, Wanasheria na Bank ya FNB iliyotoa Mkopo ambapo baada ya Mkuu wa mkoa kuagiza kufanyika uchunguzi ambapo Benki ilibaini uzembe wa baadhi ya watumishi wao wa Benki hiyo uliopelekea kasoro hiyo.
RC Makonda pia amefanikiwa kumuhakikishia makazi ya kudumu Mama Mjane Bi. Benadetha Rwendera alietakiwa kuondoka kwenye nyumba yake na kujikuta akilala nje baada ya kununua eneo na kujenga nyumba pasipokujua kuwa aliemuuzia eneo tayari alikuwa amechukuwa Mkopo Bank ya KCB jambo lililopelekea nyumba kuvunjwa na kuuzwa ambapo baada ya majadiliano baina ya RC Makonda na Bank ya KCB waliafiki kwa pamoja kumuachia mjane aendelee kuishi wakati kesi ikiendelea mahakamani na pindi hukumu itakapotoka utafanyika mgawanyo wa ardhi.
Aidha RC Makonda amesema hadi sasa Mkoa umefanikiwa kusikiliza kesi za Wananchi zaidi ya 1,028,000 ambapo Kesi zilizotatuliwa ofisini kwake ni 628,000 na kesi zilizokwenda mahakamani ni 60 ambapo Kati ya hizo kesi 17 zemeshatolewa hukumu na watu kupata haki zao chini ya usimamizi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kupitia msaada wa Mawakili waliowasimamia bila malipo.
Itakumbukwa RC Makonda aliahidi kuwasaidia wananchi wasiokuwa na uwezo wa kulipa mawakili Bure na haya Ndio matunda yake.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa