Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amepokea shehena ya Makontena 20 Kati ya 36 yenye thamani ya Shillingi Billion 2 zilizotolewa na Diaspora waishio Nchini Marekani waliounga mkono kampeni ya RC Makonda ya ujenzi wa Ofisi 402 za Walimu wa Dar es salaam.
Ndani ya Kontena hizo zipo Meza za umeme zenye hadhi ya kimataifa 2500, Meza za kawaida 2500,Viti zaidi ya 5,000,Makabati makubwa ya vitabu 1300, Ubao za kisasa (writing board) zisizotumia chaki 700 ambazo kwa kiasi kikubwa utaenda kupunguza mateso ya walimu kuumwa vifua kutokana na vumbi la chaki.
Vifaa hivyo vya kisasa vimetolewa na Jumuiya ya watanzania waishio Marekani ijulikanayo kama Sixth Region Diaspora Caucus Washington iliyomuunga mkono RC Makonda kutokana na kuguswa na kazi kubwa anayoifanya kwenye kuboresha mazingira ya walimu.
Akizungumza wakati wa kupokea makontena hayo RC Makonda amesema jumla ya kontena zilizotolewa na jumuiya hiyo ni 36 na Kati ya hiyo 20 yamefika na mengine 16 yapo njiani ambapo ameshukuru jumuiya kwa kutambua thamani ya mwalimu.
RC Makonda amesema lengo lake ni kuboresha mazingira ya walimu na kurejesha heshima yao ili wapate morali ya kufundisha wanafunzi na mwisho wa siku kusaidia taifa kuwa na wataalamu wa kutosha.
Aidha ameishukuru Bank ya Walimu kwa kusaidia kulipia usafirishaji wa makontena matatu na kuwaomba wadau kusaidia kulipia gharama za usafiri wa makontena mengine kama mchango wa kutambua thamani ya mwalimu.
Walimu walioshuhudia makontena hayo wamemshukuru RC Makonda kwa namna anavyoboresha mazingira yao ya kufanya kazi na kueleza kuwa vifaa walivyovishuhudia leo wanaamini sasa watafanya kazi kwa bidii zaidi na kuongeza ufaulu kwa walimu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa