Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo ametembelea na kukagua Maendeleo ya ujenzi wa miundombinu kwa ajili ya Showroom zote za Magari kwenye eneo Maalumu lililotengwa Kigamboni.
RC MAKONDA ameongozana na viongozi wa Taasisi mbalimbali ikiwemo TRA, SUMATRA, NSSF, Bank ya watu wa Zanzibar pamoja na Jeshi la Polis na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambao wameenda kuonyeshwa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya Ujenzi wa Ofisi.
RC MAKONDA amesema kuwa lengo la kuhamishia Showroom Kigamboni ni kufanya Kigamboni kuwa soko la Magari Africa, kuwapa Wananchi fursa ya kuchagua gari analotaka kwenye eneo moja, kuiwezesha Serikali kupata mapato na kupunguza wizi wa magari.
Akiwa kwenye eneo hilo ameshuhudia ujenzi wa miundombinu ya Barabara, Madaraja, Umeme na Maji ikienda kwa kasi kubwa.
Tayari baadhi ya Taasisi na wenye Showroom waliokabidhiwa maeneo wameanza kujenga ili kuhakikisha ifikapo January Mosi wanakuwa wamehamisha Showroom zao.
Ndani ya eneo hilo kutakuwa na ofisi za Taasisi zote zinazohusiana na biashara ya Magari ikiwemo TRA, TPA, SUMATRA, BANk, NSSF,Bima, Jeshi la Polisi, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Garage, Sheli na Wauzaji wa Vipuri vya Magari.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa