Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa PAUL MAKONDA amekabidhi Magari ya kisasa 18 kati ya 26 yaliyopelekwa Mkoani Kilimanjaro yakiwa mabovu (mkweche) kwa ajili ya kufufuliwa upya.
Magari hayo yalipelekwa Kilimanjaro yakiwa yamebebwa kutokana na ubovu lakini sasa yanarejea Dar es Salaam yakiwa mazima na mwonekano kama Magari ya UN ambapo yatakuwa na uwezo wa kubeba Askari 11 wakiwa wamekaa na silaha zao.
Akikabidhi Magari hayo kwa Jeshi la Polisi leo RC MAKONDA amesema yataenda kuhudumia wananchi kwa kuimarisha Ulinzi na Usalama jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa kilichomgusa kuboresha Jeshi la Polisi ni baada ya kuona Askari wakifanya kazi katika mazingira magumu na wakati mwingine kuvamiwa na majambazi kisha kuuwawa na kuporwa Silaha.
Aidha RC MAKONDA ameishukuru kampuni ya Rajinder Motors Ltd (RSA) kwa kumuahidi kutengeneza Magari 56 ya Polisi Dar es Salaam bila kutumia fedha za serikali (Bure).
Mhe. MAKONDA ametumia Makabidhiano hayo kutuma salamu kwa Majambazi, Vibaka na wale wenye nia ya kuvuruga Amani na Usalama kuwa kiama chao kimefika.
Amesema alipotangaza mpango wa kufufua Magari yaliyokufa wapo waliombeza lakini sasa wanajionea magari yakiwa Mapya.
Makabidhiano hayo yameshuhudiwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. ANNA MGWIRA, Kamanda wa Polisi kanda Maalumu ya Dar ea Salaam Lazaro Mambosasa na viongozi wengine wa vyombo vya Ulinzi na Usalama ambapo wamempongeza RC MAKONDA kwa ubunifu mkubwa alionao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa