Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amekabidhi kadi 220 za Bima ya Afya (Toto Afya Card) zenye thamani ya zaidi ya shilingi Million 11 kwa watoto yatima na waishio Kwenye mazingira magumu ili wapate uhakika wa matibabu mwaka mzima ikiwa ni sehemu ya Mwezi mtukufu wa Ramadhan.
RC Makonda amesema kwa kawaida Mwezi wa Ramadhan watu wamekuwa wakifuturisha watoto yatima lakini inakuwa ni chakula cha siku moja kwaiyo katika mwendelezo wa mwezi mtukufu ameona ni vyema aguse maisha ya watoto yatima kwa kuwapatia uhakika wa matibabu kwa kuwapatia Bima ya Afya ambapo ameamua kuanza na watoto 220 na baadae ataongeza wengine.
Aidha RC Makonda amesema kadi hizo zitawawezesha watoto kupatiwa matibabu Bure kwa kipindi cha mwaka mmoja katika HospitalIi yoyote hapa nchini.
Hata hivyo RC Makonda amesema watoto waliopatiwa kadi hizo hawahusiani na wale waliojitokeza kwenye Zoezi la kutafuta haki ya mtoto ambapo ameshukuru Hospital ya Regency na TMJ kwa kujitolea kutoa kadi hizo.
Sambamba na hilo RC Makonda amesema atakabidhi pia mabegi 400 yaliyosheheni vifaa vyote vya Shule kwa vituo vya watoto yatima na waishio kwenye mazingira magumu ili wawe na uhakika wa kupata masomo mwaka mzima na kuweza kutumia vyema fursa ya elimu bure.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Hospital ya Regency Dr. Kanabar Rajni na Mkurugenzi wa hospital ya TMJ Bi. Parul Chhaya kwa pamoja wamesema wameguswa kutoa msaada huo Kama sehemu ya kuunga mkono hamasa anayoitoa RC Makonda kwa wazazi kuwa na kadi za bima za afya (Toto Afya Card).
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa