Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ametoa ahadi ya kuwasomesha kuanzia kidato cha tano hadi cha sita bure wasichana 100 waliofanya vizuri kwenye masomo ya sayansi katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne ili kuongeza idadi ya wanawake wataalamu na wabobezi wa nyanja mbalimbali.
RC Makonda amesema amegundua kuwa wapo mabinti wengi waliofaulu vizuri masomo yao lakini kutokana na wazazi wao kutokuwa na uwezo wa kuwaendeleza kielimu wameishia kupoteza ndoto zao hivyo ameona ni vyema akawaendeleza.
Aidha RC Makonda ameeleza kuwa wasichana hao watagharamiwa kila kitu kuanzia ada, mabegi, vitabu na sare za shule ili wabaki na kazi moja pekee ya kusoma na kufaulu.
Hayo yote yamejiri leo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika ukumbi wa Mlimani City na kuhudhuriwa na Maelfu ya wanawake.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa