Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa PAUL MAKONDA Leo amefungua mkutano wa zoezi la utoaji wa Kingatiba (Dawa za Matende, Mabusha na Minyoo ya tumbo) kwa Mkoa wa Dar es Salaam litakalo fanyika kesho kimkoa katika Manispaa ya Kigamboni.
Mkutano huo uliohudhuriwa na Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Sehemu na Vitengo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Makatibu tawala wa wilaya, Wakurugenzi, Timu ya afya ya Mkoa , Waganga Wakuu wa Hospitali za Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam, Maofisa mbalimbali wa Serikali katika Ngazi ya Mkoa, Wilaya na Wizara ya Afya.
Awali Mganga Mkuu wa Mkoa Dr. Grace Magembe alieleza kuwa zoezi hili hufanyika kila mwaka ambapo wananchi hupewa kinga tiba dhidi ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.
Alieleza kuwa wakufunzi wote walishapewa mafunzo kuanzia tarehe 20-25/11/2017 ya uhamasishaji wa watu kunywa dawa kuanzia katika Halmashauri zetu zote. Hata hivyo huduma hii imepanuka Zaidi ambapo itafika mpaka kwenye Vituo vya mabasi, Masoko, Ofisi za Serikali, Ofisi za Kata, Wizara na Taasisi zote za Umma.
Mheshimiwa PAUL MAKONDA amesema kuwa mkakati wa utoaji wa kinga tiba unaofanyika kila mwaka ni wa muhimu sana kwani magonjwa hayo yalikuwa yamesahaulika lakini yanasababisha athari kubwa katika jamii yetu.
Amesema Juhudi na Ubunifu usaidie sana katika kuwapatia wananchi wengi kuweza kupata dawa. Aidha dawa hizo zitawasaidia katika kujikinga dhidi ya magongwa hayo. “Dawa hizi ni Safi na Salama kwa matumizi” Alisisitiza RC MAKONDA.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa