Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa miundombinu ya Barabara na Madaraja inayotekelezwa na Serikali kwenye Wilaya ya Kigamboni ambapo kukamilika kwake kutafanya Mji wa kigamboni kuwa wa kisasa zaidi.
Miongoni mwa miradi iliyotembelewa na RC Makonda ni ujenzi wa Barabara ya njia sita za magari kuelekea Daraja la Mwalimu Nyerere yenye urefu wa Km 2 pamoja Mzunguko wa Magari (Round about) yenye ukubwa wa Mita 250 kuelekea Feri Mita 250 kuelekea Kibada ambayo ujenzi wake unatarajiwa kukamilika Octoba 31 mwaka huu.
Aidha RC Makonda ametembelea ujenzi wa Barabara ya KKKT na mitaro ya maji yenye urefu wa Mita 275, Barabara ya Hospital ya Vijibweni Mita 800 kutoka Kibada,Barabara ya Kijaka-Mwasonga Km 8, Mwasonga-Kibada Km 16 Kimbiji-Pembamnazi, Daraja la Puna eneo la Buyuni na Daraja la Kibugumo Kata ya Gezaulole ambapo miradi hiyo ipo hatua za mwisho kukamilika.
RC Makonda ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa miradi hiyo na kuwahimiza TANROAD na TARURA kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati ili wananchi waendelee kufurahia matunda ya serikali ya awamu ya tano.
Pamoja na hayo RC Makonda amesema wamejidhatiti kuhakikisha Kigamboni inakuwa na Barabara za Lami, Maji ya kutosha na Umeme kwa ajili ya Viwanda, Makazi na Showroom kubwa Africa Mashariki na Kati.
TULIAHIDI NA TUNATEKELEZA.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa